• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Kombe la dunia la mpira wa kikapu, timu zaidi zaingia hatua ya 16 bora.

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:30:19

  Timu ya mpira wa kikapu ya Marekani baada ya kupata ushindi wa 93-92 katika muda wa ziada dhidi ya Uturuki, imekuwa timu ya sita kutinga hatua ya 16 bora ya mashindano ya dunia ya mpira wa kikapu (FIBA Basketball) yanayoendelea hapa China.

  Marekani imeungana na Australia, Lithuania, Jamhuri ya Dominika, Ufaransa na Brazil.

  Uturuki itakutana na Jamhuri ya Czech ambao wamemwaga Japan. Huku Brazil wao waliwafunga Greece kwa mabao 79-76, nao Australia walitinga hatua ya 16 bora kwa kuwachomoa Senegal kwa 81-68 kwenye kundi H na kuungana na Lithuania ambao wamemfungua Canada kwa 92-69.

  Ujerumani wao wamekubali kichapo toka kwa Jamhuri ya Dominika katika kundi G, nao Ufaransa wametinga hatua hiyo kwa kuwapiga Jordan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako