• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi ya mabingwa Afrika- Zahera anoa washambuliaji wake

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:31:53

  Katika kuelekea mchezo wao wa raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika, Kocha mkuu wa Yanga raia wa DRC Mwinyi Zahera, ametumia dakika 50 kuwapa mbinu za ufungaji mabao washambuliaji wake.

  Yanga inatarajiwa kuvaana na Zesco United kati ya Septemba 13 hadi 15, mwaka huu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zahera amebainisha kuwa, nguvu na akili zote amezielekeza kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi chake. Aliongeza kuwa lengo ni kuona washambuliaji hao wanafunga mabao katika michezo ijayo ya ligi na michuano ya kimataifa wanayoshiriki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako