• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RAGA: Kenya Simbas yaporomoka viwango vya raga duniani

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:32:08

  Timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya Kenya almaarufu Simbas imeporomoka kutoka nafasi moja hadi nafasi ya 34 katika viwango bora vya Shirikisho la Raga Duniani (World Rugby) vilivyotangazwa Jumatatu.

  Afrika Kusini na Namibia zinashikilia nafasi mbili za kwanza barani Afrika katika nafasi ya tano na 23 duniani, mtawalia. Zimbabwe na Kenya zinafuatana katika nafasi ya tatu na nne barani Afrika.

  Uganda imechupa hadi nafasi ya tano barani Afrika na 41 duniani baada ya kuifunga Zambia 35-28 katika mechi ya Victoria Cup jijini Lusaka. New Zealand imerejea katika nafasi ya kwanza duniani kutoka nafasi ya pili, huku Ireland ikikamata nafasi ya pili na nafasi ya tatu imesaliwa na Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako