• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wapongeza juhudi za SADC kwa ajili ya kikosi cha kikanda

  (GMT+08:00) 2019-09-04 09:38:51

  Umoja wa Afrika umezipongeza nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kutokana na juhudi zilizofanya kwa ajili ya kukiwezesha kikosi cha kikanda cha SADC kutekeleza majukumu yake chini ya mfumo wa Kikosi cha Pamoja cha Afrika ASF.

  Taarifa iliyotolewa jana na Umoja wa Afrika imesema, Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo limetafakari juu ya kikosi cha kikanda cha SADC, hasa ujenzi wa kituo cha ugavi cha kikanda cha SADC, na kutoa wito kwa kanda nyingine za Afrika kujifunza uzoefu bora wa SADC.

  Baraza hilo pia limeipongeza China kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa za kuimarisha uwezo wa Kikosi cha Pamoja cha Afrika, na hivyo kuchangia amani na utulivu barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako