• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uholanzi apendekeza Umoja wa Ulaya kujenga mfumo wa pamoja wa kuwalinda wakimbizi

    (GMT+08:00) 2019-09-04 09:41:14

    Waziri mkuu wa Uholanzi Bw. Mark Rutte jana alizisisitiza nchi za Umoja wa Ulaya kushirikiana ili kukabiliana na suala la wakimbizi na kutoa pendekezo kwa Umoja wa Ulaya kujenga mfumo wa pamoja wa kuwalinda wakimbizi.

    Bw. Rutte ameyasema hayo alipokutana na waziri mkuu wa Hellenic Bw. Kyriakos Mitsotakis ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi. Baada ya mkutano huo Bw. Rutte alisema, walifanya majadiliano kuhusu kuhimiza ongezeko la uchumi, kupanua ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili, kukabiliana na suala la wakimbizi na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Kuhusu suala la wakimbizi, Bw. Rutte alisema, Umoja wa Ulaya unapaswa kuweka shinikizo kwa nchi wanachama zisizopenda kujiunga kukabiliana na suala hilo na kujenga mfumo wa pamoja wa kuwalinda wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako