• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabalozi wa kigeni waunga mkono ombi la Kenya kuwa na kiti kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-09-04 09:43:04

    Mabalozi wa kigeni wameahidi kuunga mkono ombi la Kenya kupata kiti kisicho cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuisaidia kupandisha hadhi yake kama kituo cha kidiplomasia cha kikanda.

    Mabalozi 11 wapya ambao walikutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wakikabidhi hati zao, wamesema, wataunga mkono ombi la Kenya kushinda kiti katika chombo cha juu cha Umoja wa Mataifa kinachofanya maamuzi kuhusu amani na usalama wa dunia.

    Mabalozi hao wanaotoka Ulaya, Afrika na Asia wamesisitiza tena uungaji mkono kwa ombi hilo la Kenya la kushinda kiti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi wa Juni mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako