• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Uingereza asema ataitisha uchaguzi mkuu baada ya kushindwa bungeni

  (GMT+08:00) 2019-09-04 09:56:02

  Waziri mkuu wa Uingereza jana usiku alitangaza kuwa ataitisha uchaguzi mkuu kama wabunge leo watapiga kura ya kupinga Brexit isiyo na makubaliano.

  Taarifa hiyo ameitoa baada ya wabunge hao kupitisha mswada wa dharura leo Jumatano wa kumzuia Johnson kuitoa Uingereza kwenye umoja huo bila ya makubaliano ifikapo Oktoba 31 kwa kupiga kura 328 dhidi ya 321. Uchaguzi unaweza kufanyika Oktoba 14 lakini hadi sasa bado haijaamuliwa tarehe rasmi.

  Johnson amesema kama wabunge hao wataupigia kura mswada huo, njia pekee iliyobaki ni kuwaachia watu waamue nani atakayekwenda Brussels Oktoba 17. Amesema kama kiongozi wa Labour Jeremy Corbyn akienda Brussels, atafanya vile wanavyotaka Umoja wa Ulaya na ataingia kwenye makubaliano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako