• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema Marekani inajiaibisha kutumia vyombo vya kiserikali kuikandamiza kampuni ya China

  (GMT+08:00) 2019-09-04 18:49:14

  China inapinga kitendo cha Marekani kutumia vyombo vya kiserikali kuikandamiza kampuni ya China bila ya sababu yoyote, kitendo ambacho inaona ni cha kujiaibisha na kutofuata maadili, na pia ni kinyume na kanuni ya uchumi wa soko inayotetewa sana na nchi hiyo.

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema hayo kufuatia habari kuwa Wizara ya Sheria ya Marekani imeanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya Huawei kwa madai ya kuiba siri za kibiashara. Kampuni ya Huawei imetoa malalamiko ikisema Marekani inatumia chombo cha kiserikali kusumbua shughuli zake za kawaida.

  Bw. Geng amesema China inaitaka Marekani irekebishe kosa lake la kutumia vibaya maana ya usalama wa taifa, kuacha kuharibu jina na kutoa shutuma dhidi ya China, kuacha kuikandamizi kampuni ya China bila ya sababu yoyote na kutoa mazingira yenye ushindani wa usawa bila ya ubaguzi kwa kampuni za China zinazofanya biashara nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako