• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EWURA yatangaza bei mpya za mafuta Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-09-04 19:59:56

  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania imetangaza bei za kikomo kwa bidhaa za mafuta nchini humo zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatano Septemba 4,2019.

  Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano kwa umma wa Ewura, Wilfred Mwakalosi amesema bei za jumla na rejareja za mafuta za petroli dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka.

  Mwakalosi amesema mafuta hayo ni yale yaliyoingia kupitia bandari ya Dar es Salaam ambayo yameongezeka ukilinganisha na mwezi uliopita.

  Amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na yanayoingizwa kupitia bandari ya Tanga yameongezeka ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.Aidha amefafanua kuwa bei ya rejareja za mafuta ya taa katika baadhi ya mikoa zimetokana na gharama za mafuta hayo katika bandari ya Dar es Salaam na kusafirishwa kwenye mikoa husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako