• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Michuano ya kufuzu kombe la dunia 2022- Burundi na Tanzania hakuna mbabe

  (GMT+08:00) 2019-09-05 10:51:35

  Mchezo wa kwanza kwa wa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar 2022 ulipigwa jana uwanja wa Prince Louis Rwagasore jijini Bujumbura kati ya Burundi na Tanzania na kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

  Burundi walianza kupachika bao dakika 81 kupitia Cedric Amiss na Simon Msuva wa Tanzania alisawazisha katika dakika ya 85. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba 8 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania.

  Michezo mingine ya kufuzu kombe hilo ilipigwa katika nchi tofauti, Namibia imeifunga Eritrea 2-1, nao Lesotho na Ethiopia hakuna mbabe baada ya kutoka sare ya bila kufungana, huku Sudani Kusini nayo ikitoka suluhu ya 1-1 na Equatorial Guinea, Mauritius imekubali kipigo cha 1-0 toka kwa Msumbiji, Djibouti ikiizamisha Eswatini kwa 2-1 na Sao Tome and Principe imesalimu amri ya 1-0 kwa Guinea Bissau.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako