• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: CAF yawaruhusu Yanga kumtumia Shikalo

  (GMT+08:00) 2019-09-05 10:52:13

  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wamemruhusu kipa mkenya Farouk Shikalo kuanza kutumika kwenye ligi ya mabingwa Afrika baada ya kumpiga stop kutumika kwenye mechi za awali.

  Wachezaji wengine ambao walikosa leseni ni pamoja na straika Mcongo David Molinga na Mustapha Suleiman.

  Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa wamepata ruhusa ya kumtumia Shikalo ikiwa ni baada ya CAF kutoa leseni yake ambapo watamtumia kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Zesco United.

  Wakati huo huo Kocha mkuu wa klabu hiyo raia wa DRC Mwinyi Zahera amekanusha madai ya kupewa mechi tatu na mabosi wake ambazo akipoteza atafukuzwa kazi.

  Zahera ameeleza kuwa hajapewa mechi hizo na yanayoandikwa mitandaoni hayana ukweli wowote ule.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako