• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China asisitiza umuhimu wa kuinua kiwango cha maadili na utamaduni

  (GMT+08:00) 2019-09-05 19:29:11

  Rais Xi Jinping wa China amesisitiza jitihada za kuhimiza kampeni ya kuinua kiwango cha maadili na utamaduni ili kukilea kizazi kipya chenye uwezo wa kubeba majukumu ya kustawisha taifa tena.

  Rais Xi amewapongeza wale waliochaguliwa kuwa mifano ya kitaifa ya watu wenye maadili, na kusema sifa hizo zina maana kubwa katika kuboresha tabia za kijamii, kuongeza nguvu chanya na kuhimiza watu kujitahidi kuwa na ubora na maadili zaidi.

  Rais Xi pia amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa wazo kuu la kijamaa kuhusu thamani. Ametoa wito wa kuongeza kiwango cha maadili ya kijamii, kikazi, kifamilia na kibinafsi, ili kusaidia kutimiza ndoto ya China katika zama mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako