• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa China na Chansela wa Ujerumani wazungumza kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2019-09-05 20:01:31

  Kabla ya kuanza ziara yake ya 12 nchini China Ijumaa na Jumamosi wiki hii, Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel jana alizungumza na mwenzake wa China Bw. Li Keqiang kwa njia ya simu.

  Bibi Merkel amesema Ujerumani inatilia maanani uhusiano kati yake na China, na anatarajia kuwa katika ziara yake, nchi hizo zitaimarisha ushirikiano wao na kutoa ishara chanya kuwa nchi hizo zitadumisha uhusiano mzuri wakati zinakabiliwa na hali ya utatanishi ya kimataifa.

  Bw. Li Keqiang amesema anakaribisha ziara ya Bibi Merkel na kwamba China inapenda kushirikiana na Ujerumani kuongeza hali ya kuelewana na kuaminiana, kuimarisha ushirikiano katika sekta zote, kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, na kuendeleza vizuri uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako