• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kenyatta afungua maonyesho ya kilimo Mombasa

    (GMT+08:00) 2019-09-05 20:19:21
    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo amefungua rasmi maonyesho ya biashara na kilimo mjini Mombasa.

    Maelfu ya wakazi,wafanyabiashara wa ndani na wale wa kigeni walijitokeza katika maonyesho hayo yaliyoanza jumatano Septemba 4.

    Wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, Rais ambaye ni mdhamini wa Shirika la Maonyesho ya Kilimo nchini (ASK) alizuru vibanda kadhaa vya maonyesho, na kutoa hotuba rasmi na pia kuwatunuku waonyeshaji bidhaa na huduma waliotia fora katika maonyesho hayo.

    Maonyesho ya Kimataifa ya Mombasa ya mwaka 2019 yamevutia zaidi ya wafanyabiashara 190 wa bidhaa na huduma kutoka mataifa ya Uganda, Tanzania, Ukraine, China na Visiwani Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako