• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya PWC yaonyesha kuwa wakurugenzi wa makampuni Afrika wana wasiwasi kuhusu uchumi

    (GMT+08:00) 2019-09-05 20:19:40
    Viongozi wa biashara barani Afrika hawana matumaini kuhusu nguvu ya uchumi wa dunia na uwezo wa mashirika yao wa kuongeza mapato katika muda mrefu na mfupi,kama yalivyokuwa mwaka mmoja uliopita.

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti ya Agenda ya Biashara Afrika 2019 ilitolewa na Shirika la PWC.

    Ripoti hiyo ambayo ilizinduliwa katika Mkutano wa Uchumi Duniani ulioandaliwa jijini Cape Town Afrika Kusini ilionyesha kuwa robo wa Maafisa Wakuu watendaji barani Afrika (asilimia 25) wanaamini kuwa uchumi wa dunia utaporomoka katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

    Wasiwasi kuhusu kuhusu ukuaji wa uchumi duniani pia unavunja ujasiri wa Maafisa Wakuu Watendaji kuhusu muonekano wa kampuni zao wenyewe katika muda mfupi,huku asilimia 27 ya Maafisa hao wakisema wana imani na matarajio ya kampuni zao ya kuongeza mapato katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako