• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Mwakinyo kuzichapa Oktoba jijini Dar es Salaam

  (GMT+08:00) 2019-09-06 09:06:20

  Bondia namba moja Afrika katika viwango vya ubora uzito wa super welter raia wa Tanzania Hassan Mwakinyo, kwa mara ya kwanza atapanda ulingoni mwezi ujao katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam kuzichapa kati ya bondia Stephano Castelluccio wa Ufilipino ama Arnel Tinampay wa Italia au bondia kutoka Marekani, Urusi ama Argentina.

  Promota wa pambano hilo Jay Msangi amesema, pambano hili linatarajiwa kuwa la raundi 10 kuwania ubingwa wa super welter na tayari wamezungumza na vyama vya ngumi vya kimataifa vya WBO na IBO ili Mwakinyo agombee mkanda wa ubingwa wa vyama hivyo. Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo amesema yuko fiti na hana hofu ya kuzichapa na bondia yeyote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako