• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Bakhresa yawaonya wafanya biashara dhidi ya kutumia vifungashio vyao

    (GMT+08:00) 2019-09-06 19:09:18

    Wakurugenzi wakuu wa kampuni ya Said Salim Bakhresa & Ltd (SSB) umewatahadharisha baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia vifungashio vilivyotumika katika bidhaa za Azam na kujaza bidhaa nyingine zenye mwonekano wa kampuni hiyo na kuziuza wa wateja.

    Uongozi wa kampuni hiyo ulisema hayo kupitia kwa mkurugenzi wa uhusiano wa SSB, Hussein Sufian.

    Sufian amesema wamebaini uwepo wa baadhi ya wazalishaji wenye tabia ya kuiga na kubadilisha rangi na mwonekanao wa bidhaa za Azam kila wanapofanya mabadiliko ya bidhaa zao mbalimbali.

    Sufian ameeleza kuwa katika kukabiliana na hali hiyo, uongozi wa kampuni hiyo umeamua kubadilisha mwonekano wa bidhaa yake maarufu ya unga wa ngano unaoitwa ngano bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako