• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kuunda sera za kulinda wafanya biashara wadogo

    (GMT+08:00) 2019-09-06 19:10:08

    Serikali za Afrika zimetakiwa kuunda sera na utaratibu mzuri utakaotoa mwongozo kwa biashara ndogo ndogo na za kati katika sekta ya kilimo. Wakizungumza mjini Cape town wataalamu wa kiuchumi wamesema ni wajibu wa serikali kulinda watumizi dhidi ya bidhaa za ubora wa chini kama vile pembejeo za kilimo, mbegu, mbolea pamoja na bidhaa za chakula ambazo zinafikishwa sokoni. Wamesema endapo sera nzuri za kuwalinda wafanya biashara wadogo zitaundwa basio itakua ndio mwanzo mzuri wa kuwalinda wafanya biashara hao. Mkuu wa shirika la AGRA Daktari Agness Kalibata amesema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikipuuza utungaji wa sera nzuri za kuwalinda wafanya biashara wadogo lakini sasa ni wakati wa kuchukua hatua hiyo ili kuhakikisha watumizi wanafikiwa na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Asilimia 64 ya vyakjula vinavyotumiwa barani Afrika vinashughulikiwa na mamilioni ya wafanya biashara wadogo na wa kati jambo ambalo limewapa fura za ajira kwa familia nyingi na wakulima wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako