• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe mpya wa China kuhusu suala la Mashariki ya Kati ataka kutoa mchango kwaamani na utulivu wa eneo hilo

  (GMT+08:00) 2019-09-06 19:29:29

  Mjumbe maalum mpya wa China anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati Bw. Zhai Jun, amesema anatarajia pande zote husika zitaanzisha uhusiano wa karibu wa ushirikiano, kuhimiza mazungumzo ya amani ili kutoa mchango wa kiujenzi kwa ajili ya kuhimiza amani, utulivu na usalama wa eneo hilo.

  Bw. Zhai amesema hivi sasa hali ya eneo hilo ni mbaya na baadhi ya nchi kubwa zinaendelea kufuata mfumo wa upande mmoja na uonevu, kutoa shinikizo ya kupita kiasi, kupuuza makubaliano ya kimataifa na kusababisha athari mbaya kwa hali ya eneo hilo.

  Bw. Zhai pia amesema hali ya Mashariki ya Kati inahusu amani na utulivu wa dunia. China inaona kusimamisha mapambano mapema, kutimiza utulivu na kupata maendeleo katika eneo hilo kunahitaji jitihada za pamoja za jumuiya ya kimataifa na nchi za kanda hiyo. Pia amesema China inatarajia kuongeza mawasiliano na uratibu na pande mbalimbali na kuhimiza pande husika kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo ili kujenga mazingira tulivu na salama kwa nchi za eneo hilo kujitafutia njia yao za kujiendeleza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako