• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema Marekani kuwataka washirika wake waikane Huawei ni kitendo cha umwamba

  (GMT+08:00) 2019-09-06 19:40:04

  China inapinga Marekani kuwashawishi washirika wake kutotumia teknolojia ya kampuni ya Huawei, kitendo ambacho inasema ni cha sera ya umwamba na kuingiza siasa kwenye suala la biashara. Habari zinasema makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence ambaye yuko ziarani nchini Iceland, amewaambia wanahabari kuwa nchi hizo mbili zitajadili wasiwasi wa Marekani katika ujenzi wa mtandao wa 5G na kutoa wito kwa Iceland na washirika wote wa Marekani kukataa teknolojia ya Huawei.

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China inaitaka Marekani iache kutumia vibaya maana ya usalama wa taifa na vyombo vya kiserikali kuikandamiza kampuni ya China na kutoa mazingira yenye ushindani wa usawa bila ubaguzi kwa kampuni za China zinazofanya biashara nchini humo.

  Wakati huohuo, alipojibu shutuma zilizotolewa na waziri mkuu wa Canada Bw. Justin Trudeau kuwa China inawakamata ovyo raia wa Canada ili kutimiza malengo ya kisiasa ya ndani na nje ya nchi, Bw. Geng amesema Canada inafurahia kuwa kibaraka wa Marekani na kumshikilia raia wa China Bibi Meng Wanzhou asiyekiuka sheria ya Canada. Amesisitiza kuwa China inafanya mambo kwa mujibu wa sheria bila ya kutumia vigezo viwili, kitendo ambacho ni kanuni inayofuatwa na nchi nyingi duniani, lakini Canada si moja ya nchi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako