• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wazitaka Somalia na Kenya kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa mpaka wa baharini

  (GMT+08:00) 2019-09-06 20:18:50

  Umoja wa Afrika umetoa mwito kwa Somalia na Kenya kutafuta na kuongeza mashirikiano kwa lengo la kutafuta njia nzuri na endelevu ya kuondoa mgogoro wao wa mpaka.

  Kwenye mkutano uliofanyika jana, baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, limejadili mgogoro wa mpaka wa baharini kati ya nchi hizo mbili kwenye makao makuu mjini Addis Ababa, na kuzitaka nchi hizo kuepuka kitendo chochote kinachoweza kutishia ujirani mwema uliopo kati ya nchi hizo mbili.

  Somalia na Kenya zimekuwa na mgogoro wa mpaka wa muda mrefu, kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa laki moja za mraba.

  Somalia ilifikisha mgogoro huo kwenye mahakama ya kimataifa ICJ mwaka 2014, lakini Kenya ilipinga uhalali wa mahakama hiyo, na kutaka suala hilo litatuliwe kwa njia ya mazungumzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako