• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa maombolezo kwa kufariki kwa Mugabe

  (GMT+08:00) 2019-09-06 20:38:58

  Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 95.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amemtaja marehemu Mugabe kama kiongozi na mwanasiasa aliyekuwa hodari katika ukombozi wa Zimbabwe. Pia alijikita kwenye kulinda uhuru wa taifa, kupinga uingiliaji wa nje, na kuhimiza uhusiano wa kirafiki wa ushirikiano kati ya China na Zimbabwe na China na Afrika. China imetoa salamu za rambirambi kutokana na kifo chake na kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Zimbabwe, na familia za Bw. Mugabe.

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe aliyekuwa ziarani nchini Afrika Kusini, amekatisha ziara yake na kurudi nchini Zimbabwe kufuatia kifo cha Bw. Mugabe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako