• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yaitaka Afrika mashariki kutenga rasilimali za kukabiliana na ukame

  (GMT+08:00) 2019-09-07 17:57:48

  Kenya imezitaka serikali za Afrika Mashariki kutenga rasilimali za ziada ili kuongeza juhudi za kupunguza ukame ambao umekuwa tukio la kawaida kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

  Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa kupambana na ukame Waziri wa ugatuzi na maeneo kame wa Kenya Eugene Wamalwa amesema nchi wanachama wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD zinalazimika kuona ukame kama hatari inayohitaji kudhibitiwa. Amezitaka nchi hizo kutekeleza mipango ya kusaidia jamii ziishi maisha ya kawaida na kunufaika na maliasili.

  Amesema nchi za kanda hiyo ni lazima zitenge bajeti na pia kutunga sera na miongozo ya kuhakikisha kwamba dharura za ukame haziwi tena tishio, na kupendekeza kufanya uratibu kwa ufanisi kutoka ngazi ya mashinani, taifa na kikanda ili kumaliza tatizo la ukame.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako