• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Tanzania na Uganda wazindua jengo la Mwalimu Nyerere lililojengwa na China

    (GMT+08:00) 2019-09-07 17:58:22

    Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni jana walizindua Jengo la Mfuko wa Mwalimu Nyerere, MNF lililojengwa na kampuni ya uhandisi ya China CRCEG.

    Marais wote wawili wameipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri ya kujenga jengo linalovutia. Jengo hilo lenye ghorofa 30 ni mradi wa ushirikiano kati ya CRCEG, MNF na Shirikisho la Fedha la Kimataifa ambao umegharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 150. Akiongea kwenye uzinduzi huo rais Magufuli amesema shughuli hiyo ya uzinduzi wa jengo inakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 20 tangu muasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere afariki dunia. Ameongeza kuwa changamoto kubwa inayoikabili Tanzania ni kuheshimu kile alichokipigania Nyerere. Naye Museveni amesema Nyerere atakumbukwa daima kwa mapambano yake dhidi ya ukoloni nchini Afrika Kusini.

    Wakati huohuo balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke amesema uzindizi wa jengo hilo ni kumbukumbu nzuri ya Mwalimu Nyerere, na pia linaongeza urithi wa mshikamano wa muda mrefu na usiovunjika na urafiki kati ya China na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako