• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ubalozi wa Afrika Kusini nchini China waadhimisha Mwezi wa Urithi wa Afrika Kusini na Mwezi wa Utalii

  (GMT+08:00) 2019-09-07 18:01:51

  Ubalozi wa Afrika Kusini nchini China leo umeandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuadhimisha Mwezi wa Urithi wa Afrika Kusini, ambapo mwezi huu wa Septemba pia wanasherehekea Mwezi wa Utalii. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Kudai, kurejesha na kusherehekea urithi wa kuishi.

  Mbali na burudani safi ya muziki wa jadi wa Afrika Kusini pia yamefanyika maonesho ya bidhaa mbalimbali za Afrika Kusini ambayo yamehudhuriwa na Waafrika Kusini wanaoishi na kufanya kazi hapa China pamoja na Wachina.

  Akifungua maonesho hayo balozi wa Afrika Kusini nchini China Bi. Dolana Msimang anasema,

  "Leo tupo hapa kwa sababu kwa Afrika Kusini mwezi huu ni muhimu sana, kwani tunasherehekea mwezi wa urithi na pia tunasherehekea mwezi wa utalii. Mwezi wa urithi unasherehekea utamaduni wetu kama taifa na utamaduni wetu kama bara".

  Akiongea kuhusu vurugu zilizotokea hivi karibuni, wenyeji kuwashambulia wageni kutoka nchi za Afrika Bi Msimang anasema,

  "Afrika Kusini imekumbwa na matukio yasiyo ya kufurahisha wiki iliyopita, lakini tunawahakikishia Waafrika kwamba, bara la Afrika ni letu sote, na Afrika Kusini ni yetu sote. Lakini ninachotaka kusisitiza zaidi ni kwamba changamoto iliyotokea kwenye nchi yetu inatuathiri sote, kwa sababu sote tunahusika na hili".

  Lengo kuu la maonesho hayo ni kutoa jukwaa kwa waingizaji wa bidhaa za chakula na vinywaji kutoka Afrika Kusini kuonesha bidhaa zao kwa Wachina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako