• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kissinger asema kutatua masuala kwa ushirikiano ni majukumu ya pamoja ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-09-07 18:03:52

    Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Alfred Kissinger amesema anaamini siku zote kuwa kutatua masuala kwa njia ya ushirikiano ni majukumu ya pamoja kwa China na Marekani juu ya amani na maendeleo ya dunia.

    Kissinger amesema China na Marekani ni nchi zenye uwezo mkubwa katika kuhimiza maendeleo na amani ya dunia kwenye sekta za teknolojia, uzoefu wa kisiasa na historia. Hata hivyo, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili unakumbwa na changomoto kubwa kutokana na kwamba zina historia na utamaduni tofauti.

    Ameongeza kuwa ni bahati kwake kushuhudia kipindi cha miaka 40 tangu nchi mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi. Anaamini siku zote kuwa ni majukumu ya pamoja ya pande zote mbili, kutatua masuala kwa njia ya ushirikiano, ili kuhimiza amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako