• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika watoa mwito wa kuondolewa vikwazo dhidi ya Sudan

  (GMT+08:00) 2019-09-08 17:06:53

  Umoja wa Afrika umetoa mwito kwa nchi mbalimbali kuondoa vikwazo vya ushiriki wa Sudan kwenye mambo ya Umoja wa Afrika. Taarifa iliyotolewa jana na baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, imesema baraza hilo limeamua kuondoa vikwazo vya kuizuia Sudan kushiriki kwenye shughuli za umoja huo, na kuwataka wadau wengine kufanya hivyo.

  Baraza pia limezitaka nchi zinazohusika kuondoa vikwazo vyote vya kiuchumi na kifedha, ikiwa ni pamoja na kuiondoa nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kwa mtazamo wa kuhimiza shughuli za uchumi na uwekezaji kutoka nje.

  Baraza hilo pia limesema linaiunga mkono serikali ya mpito ya Sudan na kuihimiza pamoja na wadau wengine, kufanikisha uchaguzi huru wa bunge na urais.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako