• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaeleza wasiwasi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-09-08 17:07:12

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR limeeleza wasiwasi wake kufuatia kutokea tena kwa matukio ya mashambulizi dhidi ya wageni ikiwa ni pamoja na wakimbizi na waomba hifadhi.

    Shirika hilo limesema limepokea simu kadhaa kutoka kwa wakimbizi na waomba hifadhi walioathiriwa hasa kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia na Somalia, ambao wana hofu kurudi nyumbani kutokana na vurugu.

    Habari zinasema baadhi ya maduka yanayomilikiwa na wageni yameporwa na kuharibiwa.

    Naibu mkurugenzi wa UNHCR nchini Afrika Kusini Bw. Leonard Zulu amesema mpango uliopitishwa hivi karibuni nchini humo unaolenga kukabiliana na chuki dhidi ya wageni unapaswa kutekelezwa, ili kuzuia na kushughulikia vitendo vya chuki vya baadaye.

    Mapambano kati ya wageni na wenyeji yamesababisha vifo vya watu 10, wawili wakiwa ni wageni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako