• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waajiriwa wenyeji wa reli ya SGR Kenya wafikia asilimia 80

  (GMT+08:00) 2019-09-08 17:07:31

  Meneja mkuu wa kampuni ya China inayosimamia uendeshaji wa reli ya SGR ya Kenya Bw. Li Jiuping, amesema hadi sasa wamefanikisha kuajiri wenyeji kwa asilimia 80, na kusema awamu ya kwanza ya mradi huo inaelekea kutimiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa hadi mwaka 2022, asilimia 90 ya wafanyakazi wake watakuwa wenyeji.

  Akiongea kwenye sherehe moja ya kutoa vyeti vya uteuzi kwa watendaji wakuu, Bw. Liu amesema kwenye baadhi ya idara tayari wamefikia au kuvuka malengo.

  Maofisa wanne watendaji wenyeji walioteuliwa, ikiwa ni pamoja na naibu mkurugenzi mkuu na meneja masoko wa mizigo, wanaungana na zaidi ya wakenya 200 kwenye uendeshaji wa reli hiyo, ambao wako kwenye ngazi ya kuanzia kiongozi wa kikundi hadi mameneja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako