• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping aomboleza kifo cha Robert Mugabe

  (GMT+08:00) 2019-09-08 17:43:56

  Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pole kwa mwenzake wa Zimbabwe Bw. Emmerson Mnangagwa kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe.

  Kwenye salamu zake rais Xi kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, ametoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Zimbabwe na familia ya Bw. Mugabe.

  Rais Xi anasema Bw. Mugabe alikuwa mwanasiasa hodari na kiongozi wa ukombozi wa Zimbabwe na bara la Afrika. Bw. Mugabe aliwahi kufanya ziara nyingi nchini China, na kutoa mchango mkubwa katika kuhimiza urafiki na ushirikiano kati ya China na Zimbabwe, na China na Afrika. Anasema kifo chake ni hasara kubwa kwa watu wa Zimbabwe, na wachina pia wamepoteza rafiki mkubwa wa miaka mingi. Rais Xi anaongeza kuwa, China inathamini urafiki na undugu kati yake na Zimbabwe, inapenda kuendelea kupanua na kuhimiza ushirikiano kati ya pande mbili kwenye sekta mbalimbali, na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na Zimbabwe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako