• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Tanzania mwendo mdundo, yatinga hatua ya makundi kwa kuichapa Burundi

  (GMT+08:00) 2019-09-09 08:31:44

   

  Taifa Stars ya Tanzania jana imewapa furaha watanzania si tu mashabiki waliofurika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam bali hata walio sehemu mbalimbali nje ya jiji hilo.

  Shangwe hiyo ni baada ya Stars kuifungashia virago Burundi kwa penalti 3-0 kufuatia mchezo wa marudiano wa kusaka kufuzu hatua ya makundi ya kombe la dunia 2022 kumalizika kwa sare ya 1-1.

  Mchezo huo ulikuwa wa dakika 120 ambapo golikipa wa Tanzania Juma Kaseja Juma alikuwa kinara wa mechi kwa kuokoa mkwaju wa penalti ulioipa Tanzania ushindi.

  Michezo mingine ilikuwa kati ya Ethiopia na Lesotho, timu hizo zimemaliza kwa sare ya 1-1, Equatorial Guinea imechomoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini, nao Sierra Leone imewafunga Liberia 1-0.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako