• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema ina haki ya kutoendelea kutimiza baadhi ya ahadi zake ya makubaliano ya nyukilia

    (GMT+08:00) 2019-09-09 08:32:54

    Maafisa wa Iran wamesema Iran ina haki ya kutoendelea kutimiza baadhi ya ahadi zake za makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 (JCPOA) wakati ambapo maslahi yake hayaheshimiwi na pande za makubaliano.

    Akifafanua uamuzi huo jana alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Cornel Feruta, waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alisema hatua ya Iran kupunguza ahadi zake ni halali na inaruhusiwa kwenye makubaliano, katika kifungu cha 36. Amesema hatua hiyo ya Iran ni jibu la kushindwa kwa Ulaya kutimiza ahadi zao za kulinda maslahi ya Iran kwa kisingizio cha kujitoa kwa Marekani kwenye makubaliano hayo.

    Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema uamuzi wa Iran wa kurutubisha uranium ni jibu baya baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano, na kusisitiza kuwa mazungumzo bado yako wazi ili kupunguza hali ya wasiwasi na kuheshimu kwa ukamilifu ahadi za makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako