Michezo mbalimbali ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya 2020 imechezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Ujerumani haitosahau kipigo cha mabao 4-2 wakiwa nyumbani kwao toka kwa Croatia.
Matokeo mengine, Denmark na Georgia zimetoka suluhu ya bila kufungana, huku Uswisi imeishushia kipigo cha maana cha 4-0 Gibraltar, nayo Romania imeifunga 1-0 Malta, nayo Uhispania imetoa kichapo cha paka mwizi cha 4-0 kwa visiwa vya Faroe, Uswidi wao wametoka sare ya bila kufungana na Norway, na katika kundi J Finland wamezamishwa kwa goli 1-0 na Italia, huku Greece wakitoka sare ya 0-0 na Liechtenstein.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |