• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afghanistan yalitaka kundi la Taliban lisimamishe mapambano na kufanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-09-09 09:15:17

    Ikulu ya Afghanistan jana ilitoa taarifa ikilitaka kundi la Taliban lisimamishe mapambano na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na serikali, ili kutimiza amani.

    Serikali ya Afghanistan imesema, mazungumzo yoyote hayatapata matokeo yanayotarajiwa bila ushiriki wa serikali ya Afghanistan. Hapo awali serikali ya Marekani ilifanya mazungumzo na kundi la Taliban kwa duru nyingi, na pande hizo mbili zikafikia rasimu ya makubaliano. Kundi la Taliban lilishikilia kusema kuwa serikali ya Afghanistan ni kibaraka kinachotumikishwa na Marekani, hivyo limekataa kufanya nayo mazungumzo ya moja kwa moja.

    Muda mfupi kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo, rais Donald Trump alitangaza kuacha mazungumzo na kundi la Taliban, baada ya shambulizi lililofanywa na kundi hilo mjini Kabul na kusababisha vifo vya watu 12 akiwemo askari mmoja wa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako