• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda ataka kupanua ushirikiano na China

    (GMT+08:00) 2019-09-09 09:39:13

    Rais Paul Kagame wa Rwanda amekutana na mkuu wa mkoa wa Zhejiang wa China Bw. Yuan Jiajun na kueleza matumaini yake kuwa, Rwanda na China zitapanua ushirikiano kufuatia Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Pia amekaribisha makampuni ya mkoa wa Zhejiang, China kuongeza uwekezaji nchini Rwanda katika sekta za miundombinu, kilimo, uzalishaji, biashara ya mtandaoni, utalii na nyinginezo, na kuisaidia nchi yake kuendeleza sekta ya uzalishaji na kujenga miji ya kisasa. Naye Bw. Yuan ameahidi kuhimiza ushirikiano halisi kati ya mkoa wa Zhejiang na Rwanda, na kuchangia ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako