• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muktano wa uzinduzi wa Mradi wa Satelaiti No. 2 wa Misri wafanyika mjini Cairo

    (GMT+08:00) 2019-09-09 18:12:21

    Mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa Satelaiti No. 2 wa Misri ambao ulifanyiwa utafiti na kuendelezwa kwa pamoja na China na Misri ulifanyika jana huko Cairo, Misri. Mradi huo utatumiwa katika mipango miji, maliasili baharini, hali ya hewa na kilimo nchini Misri.

    Mradi wa Satelaiti No. 2 wa Misri ni moja kati ya miradi muhimu ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kati ya China na Misri, pia ni moja kati ya miradi halisi ya utekelezaji wa mipango minane iliyowekwa kwenye Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. Mwenyekiti mtendaji wa Idara ya safari za anga ya juu ya Misri Bw. Mohammed El-Koosy na balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang wamehudhuria mkutano huo.

    Bw. El-Koosy amesema, Misri ikiwa nchi ya kwanza iliyoanzisha ushirikiano na China katika sekta ya satelaiti chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ujenzi wa mradi huo utachangia katika kuinua kiwango cha ushirikiano wa teknolojia za anga ya juu kati ya nchi hizo mbili. Anasema:

    "Uhusiano wa kibalozi kati ya Misri na China umekuwa na historia ya zaidi ya miaka 60. Kabla ya mradi wa satelaiti No. 2, pande hizo mbili zilishirikiana kukamilisha ujenzi wa kituo cha majaribio ya satelaiti cha Misri. Natarajia kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili haswa katika sekta ya ushirikiano wa safari ya juu na sayansi na teknolojia utazidi kupanuka katika siku za baadaye."

    Mwezi Septemba mwaka 2014, zikishuhudiwa na viongozi wa China na Misri, pande hizo mbili zilisaini mkataba wa kuanzisha ushirikiano wa satelaiti, na China inashughulikia mradi wa kituo cha majaribio. Meneja wa mradi huo Ahmed El-Raffie amesema, mradi huo utakuwa mfano mzuri wa kuigwa katika ushirikiano kati ya China na Misri kwenye sekta ya teknolojia ya anga ya juu, ambao matumizi ya satelaiti kwenye mradi huo yataisaidia Misri kupata maendeleo katika ngazi mbalimbali.

    Balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang ameeleza kuwa, mradi wa ushirikiano wa satelaiti kati ya China na Misri utachangia katika kuinua hadhi ya Misri kwenye kanda hiyo hata dunia nzima. Anasema:

    "Mradi wa ushirikiano wa satelaiti kati ya China na Misri utachangia kuongeza neema ya wananchi wa Misri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako