• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa mpito wa Algeria atoa mwito wa kuwepo kwa mamlaka huru ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2019-09-09 19:41:05

    Rais wa mpito wa Algeria Bw. Abdelkader Bensalah, ametoa mwito wa kuundwa kwa mamlaka huru ya uchaguzi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa rais.

    Taarifa kutoka ikulu imesema Bw. Bensalah ametoa maoni hayo baada ya kupokea ripoti yenye mapendekezo yaliyokusanywa kutokana na majadiliano na vyama vya siasa, jumuiya za kiraia, watu mashuhuri wa taifa, na wawakilishi na harakati za umma.

    Ripoti hiyo pia ina mapendekezo ya kupitia upya sheria ya uchaguzi, kutoa uhakikisho wa uchaguzi huru na wa haki, na kuondoka kwa baraza la mawaziri la sasa linaloongozwa na waziri mkuu Bw Nourredine Bedoui.

    Serikali ya sasa ya Algeria inataka uchaguzi ufanyike haraka ili kuondoa msukosuko wa kisiasa, ulioanza mwezi Februari kwa maandamano yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw.Abdelaziz Bouteflika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako