• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtu mmoja ameuawa na wawili wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu mjini Mogadishu

  (GMT+08:00) 2019-09-09 19:41:44

  Mtu mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa kwenye milipuko wa bomu uliotokea leo mjini Mogadishu.

  Ofisa mmoja wa Polisi amesema mlipuko huo umetokana na bomu la kutengenezwa kienyeji, lililotegwa kwenye gari ya ofisa wa polisi. Ofisa huyo amethibitisha kifo na majeruhi ya watu hao, na kusema pia kituo cha mafuta kilichokuwa karibu kimeharibiwa.

  Shambulizi hilo linafuatia mashambulizi kama hayo yanayofanywa mjini Mogadishu, tangu kutokea kwa kifo cha meya wa mji wa Mogadishu, aliyeuawa kwenye shambulizi la bomu la kujitoa mhanga ofisini kwake. Mpaka sasa hakuna kundi lililotaja kuhusika na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako