Watu zaidi ya 29 wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea kaskazini mwa Burkina Faso.
Mashambulizi hayo yote yalitokea mkoani Sanmatenga, kaskazini mwa nchi hiyo. Lori moja lililobeba watu na mizigo lilikanyaga bomu na kusababisha vifo vya raia 15 na wengine sita kujeruhiwa. Wakati huohuo, watu 14 wameuawa wakati wapiganaji wakiwashambulia wapanda baiskeli waliokuwa wakisafirisha chakula.
Serikali imeapa kuchukua hatua kuepusha kutokea tena kwa matukio kama hayo, huku ikisema imeimarisha nguvu ya kijeshi katika eneo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |