• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Thamani ya biashara na nje ya China yaongezeka kwa utulivu

  (GMT+08:00) 2019-09-09 20:17:16

  Katika miezi minane ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya jumla ya mauzo na oda ya bidhaa kutoka nje ya China imefikia dola trilioni 2.8 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.6 likilinganishwa na mwaka jana. Hii inamaanisha kuwa hali ya ujumla ya uchumi wa China inaelekea upande mzuri, ikionesha mustakabali mkubwa wa kiuchumi.

  China kushikilia kithabiti ufunguaji mlango kumetia nguvu kubwa kwenye maendeleo ya biashara na nje. Wakati huohuo, nguvu ya maendeleo ya ndani ya makampuni ya China inazidi kuongezeka na kutoa nguzo muhimu kwa biashara hizo.

  Kutokana na mazingira ya nje yanayokabiliwa na hali isiyo na uhakika, ongezeko la biashara na nje ya China litasaidia makampuni hayo kuzidi kuharakisha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kuinua thamani ya ziada ya bidhaa, kuongeza ufanisi wa utengenezaji na kuimarisha uwezo wa kukinga hatari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako