• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • COMESA kufanya mazungumzo juu ya kuikomboa sekta ya huduma wiki ijayo

  (GMT+08:00) 2019-09-10 08:18:44

  Wataalamu wa kiufundi kutoka nchi wajumbe wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) wanatarajiwa kukutana wiki ijayo nchini Zambia kujadili namna ya kuikomboa sekta ya huduma.

  Akiongea kwenye semina ya vyombo vya habari ya Kamati ya Ushindani ya COMESA, mtafiti mwandamizi wa kitengo cha biashara na forodha wa COMESA Benetict Musengele amesema nchi wajumbe 21 wameweka kipaumbele kwenye huduma zinazohusiana na biashara ya mawasiliano, usafiri, fedha, utalii, nishati, biashara na ujenzi, na uhandisi. Amebainisha kuwa wana nia ya kuboresha biashara ya huduma kwasababu ya mchango mkubwa inaotoa katika kugeuza malighafi kuwa bidhaa iliyokamilika.

  Ameongeza kuwa matokeo ya mkutano wa wataalamu wa kiufundi yatapelekewa kwenye mkutano wa baraza la mawaziri wa COMESA utakaofanyika mwishoni mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako