• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika inahitaji karibu dola bilioni 5 za Kimarekani kila mwaka kwa ajili ya miundo mbinu ya TEHAMA

  (GMT+08:00) 2019-09-10 08:19:04

  Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa katika Afrika (ECA) imebainisha kuwa bara la Afrika linahitaji karibu dola bilioni 5 za Kimarekani kila mwaka, ili kuendeleza miundo mbinu yake ya Tehama wakati ambao miundombinu ya kidijitali barani humo iko nyuma duniani.

  Kauli hiyo imetolewa jana na mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Takwimu katika ECA Oliver Chinganya. Amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundo mbinu ya Tehama barani Afrika ili kuongeza kasi, ukubwa na umadhubuti wake. Amesema wanapojadili miji ya kisasa na ya kidijitali ni muhimu pia kukumbuka kwamba labda ni theluthi moja tu ya Waafrika wanaopata huduma za internet na nusu yao wana simu za mkononi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako