• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika yaendelea kustawi

    (GMT+08:00) 2019-09-10 08:34:14

    Kiongozi wa ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Balozi Liu Yuxi jana kwenye semina ya ushirikiano kati ya China na Afrika amesema tangu mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC ufanyike mwezi Septemba mwaka 2018, mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika yanaendelea kustawi.

    Bw. Liu amesema katika mwaka mmoja uliopita nchi 44 za Afrika na kamati ya Umoja wa Afrika zimesaini nyaraka za ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na China. Thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imefikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 200, na China imekuwa mwenzi mkubwa wa kibiashara wa Afrika katika miaka 10 iliyopita.

    Bw. Liu pia amesema, shirika la ushirikiano wa maendeleo wa kimataifa la China limetangaza kutoa msaada wa kibinadamu katika nchi za DRC, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini kutokana na maambukizi ya Ebola, na kushirikiana na WHO na Umoja wa Afrika katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako