• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande zinazopambana nchini Sudan Kusini zakubaliana kuharakisha uundaji wa jeshi la umoja

    (GMT+08:00) 2019-09-10 09:14:48

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa waasi Riek Machar jana wamekubaliana kuharakisha ukaguzi na uandikishaji wa vikosi vyao, ambavyo vitaunda jeshi la umoja lenye askari 83,000, ili kulinda usalama wa nchi hiyo.

    Henry Odwar, naibu mkuu wa kundi kuu la uasi la SPLM-IO nchini Sudan Kusini linaloongozwa na Machar, amesema Bw. Machar kuweza kufika Juba na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na rais Kiir kutasaidia kuharakisha mipango ya usalama ambayo ni pamoja na uwekaji wa vikosi.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Kusini Martin Elia Lomuro amesema, maendeleo ya hivi karibuni yanaonesha kuwa pande hizo mbili zinaweza kuunda serikali ya umoja ya mpito inayosubiriwa sana kabla ya tarehe 12, mwezi Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako