• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika waomboleza kifo cha mkuu wa jeshi la akiba la Afrika

  (GMT+08:00) 2019-09-10 09:23:24

  Umoja wa Afrika umeeleza masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Meja Jenerali Trust Mugoba, mkuu wa Jeshi la Akiba la Afrika ASF lililo chini ya Tume ya Umoja huo. Mugoba, aliyekufa Ijumaa mjini Harare baada ya kuugua kwa muda mfupi, alikuwa mkuu ya majeshi ya Zimbabwe kabla ya kujiunga na Umoja wa Afrika na kuwa mkuu wa ASF tangu mwaka 2017.

  Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Mahamat Faki na Kamishna wa Umoja huo anayeshughulika na Amani na Usalama Smail Chergui wamesema kwenye taarifa kuwa Jenerali Mugoba ameonyesha moyo mzuri wa kujitolea na heshima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako