• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Maamuzi ya Solskjaer yaanza kukosolewa

  (GMT+08:00) 2019-09-10 09:28:22
  Uamuzi wa kocha wa mashetani wekundu wa Uingereza Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer wa kugawa sawa majukumu ya kupiga mikwaju ya penalti kikosini mwake, umetajwa kuwa ni mambo ya kitoto na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Matt Le Tissier.

  Man U ilikosa penalti mfululizo katika mechi dhidi ya Wolves na Crystal Palace mapema msimu huu baada ya Paul Pogba na Marcus Rashford kushindwa kufunga mikwaju ya penalty. Kutokana na kukosa huko, Solskjaer alilazimika kufafanua kuwa wawili hao wataamua wenyewe nani apige penalti msimu huu, hali ambayo Le Tissier anaona ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako