• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Afrika Kusini alaani vurugu zilizotokea nchini humo

  (GMT+08:00) 2019-09-10 10:18:51

  Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amelaani vikali vurugu zilizotokea huko Johannesburg siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu wawili, akisema huu ni uhalifu dhidi ya ustawi wa Afrika Kusini.

  Watu wawili waliuawa baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu na kikundi cha wakazi wenye silaha katika mtaa wa kibiashara katikati mwa Johannesburg.

  Rais Ramaphosa amesema serikali haitavumilia vitendo vya kukiuka sheria na ghasia kuvuruga usalama na maisha ya mamilioni ya raia wa Afrika Kusini na wageni wengi nchini humo wanaofuata sheria na kuwa na haki ya kuendesha maisha na biashara zao kwa amani. Ameongeza kuwa vurugu hizo zimeathiri vibaya uchumi.

  Watu 12 wameuawa tangu kutokea kwa vurugu dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako