• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Zimbabwe yatangaza mpango wa mazishi ya Mugabe

  (GMT+08:00) 2019-09-10 10:19:18

  Serikali ya Zimbabwe imetangaza mpango wa mazishi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Robert Mugabe aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.

  Kwenye mkutano na wanahabari, waziri wa habari wa Zimbabwe bibi Monica Mutsvangwa amesema, mwili wa Bw. Mugabe unatarajiwa kuwasili nchini humo Jumatano, na Alhamisi na Ijumaa utapelekwa kwenye Uwanja wa Michezo ya Rufaro mjini Harare, ili watu wamtolee Mugabe heshima zao za mwisho, na Jumamosi utakuwa kwenye Uwanja wa Michezo ya Kimataifa, ili wanadiplomasia, mabalozi wa nchi za nje, na wageni waheshimiwa wengine wapate kuuaga mwili wa Bw. Mugabe.

  Bibi Mutsvangwa amesema mazishi yatafanyika tarehe 15, na sehemu itatangazwa baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako