• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yashiriki kwenye Maonyesho ya kilimo ya kimataifa ya Sahara

    (GMT+08:00) 2019-09-10 18:44:28

    Maonyesho ya 32 ya kilimo ya kimataifa ya Sahara yamefunguliwa mjini Cairo nchini Misri, ambayo yamevutia makampuni takriban 210 kutoka nchi na sehemu zaidi ya kumi duniani, ikiwa ni pamoja na Misri, Hispania, Italia, Uturuki na nyinginezo. Makampuni 73 ya China pia yanashiriki kwenye maonyesho hayo.

    Maonyesho hayo yameandaliwa na Kampuni ya Informa, na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kilimo, vifaa na teknolojia za China, na makampuni ya China yanayoshiriki kwenye maonyesho hayo yanahusiana na sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mbolea, dawa za kemikali za kilimo, mashine za kilimo na umwagiliaji wa majengo ya kioo ya kuhifahdi mimea.

    Kiongozi wa kampuni ya China CCCMC Bw. Jianghui amesema makampuni ya China yanapenda kufanya biashara na ushirikiano na makampuni ya Afrika, Mashariki ya Kati na Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako