• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Nigeria wasisitiza kuwa shughuli za kundi la kiislam zimepigwa marufuku

  (GMT+08:00) 2019-09-10 19:33:20

  Serikali ya Nigeria imesisitiza kuwa shughuli za kundi la Harakati za Kiislamu la Nigeria (IMN) zinaendelea kupigwa marufuku kwa mujibu wa amri ya mahakama iliyotolewa Julai 26.

  Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nigeria Mohamed Adamu amesema mikusanyiko yote ya kundi hilo inaendelea kuwa haramu na itachukuliwa kama ni vitendo vya kigaidi.

  Bw. Adamu amesema kwa sasa polisi wameweka mkazo kwenye kuwafuatilia baada ya wanachama wa kundi hilo, wenye nia ya kuandaa maandamano ya nchi nzima, kwa lengo la kuvuruga amani, utulivu na usalama wa nchi. Amesema amewaagiza polisi katika majimbo yote, na mji mkuu kuzuia maandamano yaliyopangwa na wafuasi wa kundi la IMN.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako